Shamba Darasa
MKULIMA SMART INITIATIVES(MKUSI) ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yaani NGO yenye makao yake makuu jijijni Dodoma.
DIRA: Kuona kila mtanzania akipata chakula cha kutosha,salama na chenye viini lishe muhimu.
Malengo:
1. Kutoa taarifa muhimu za chakula kama vile bei za vyakula masokoni,hali ya hewa n.k
2.Kutoa mafunzo kwa njia ya semina,kozi fupi,makongamano,warsha na mashamba darasa
3.Kutoa huduma ya ushauri na ugani kwa wakulima,wafugaji na watanzania wote kwa ujumla ili kuzalisha chakula cha kutosha na kwa gharama nafuu.
4.Kusimika miundo mbinu mbalimbali ya kilimo na ufugaji kwa ajili ya mashamba darasa.
Ili kufikia malengo hayo njia zifuatazo zitatumika:-
Kutumia TEHAMA/ICT kama kifaa muhimu cha kupeleka tahaarifa kwa walengwa kama vile:-
1.Mitandao ya kijamii facebook,Youtube,whatup n.k
2.Radio za kijamii na televisheni
3.Tovuti ya MKUSI
4.Majarida na vijitabu.
Call/Whatup +255 713 178 868 au 0764915692.
Email:info@mkusi.org
Website www.mkusi.org